Story by Ephie Harusi –
Idadi ya wakaazi wanaojitokeza kupokea chanjo ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya Corona katika eneo bunge la Malindi imepungua kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na hapo awali.
Ni kauli iliyotolewa na Afisa wa Afya anayesimamia hospitali ya Malindi Job Gayo aliyesema hatua hiyo imetokana na wakaazi wengi wamepoteza ari ya kupata chanjo hiyo.
Akizungumza na Wanahabari baada ya kupokea vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona kutoka kwa Wakfu wa Aga khan mjini Malindi Gayo amewataka wakaazi kujitokeza kupata chanjo.
Kwa upande wake Msimamizi wa miradi katika wakfu wa Aga Khan Aquinius Mungatia amesema hospitali nyingi za kaunti zinakumbwa na changamoto za kupata vifaa vya kujikinga na mambukizi ya corona ndiposa wakfu huo amechukua hatua hiyo huku akiwataka wananchi kuzingatia masharti ya kujikinga.
Hospitali hiyo imepokea jumla ya vifaa 9,068 vya kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona vilivyo gharimu takriban shilingi milioni 4.