Story by Ephie Harusi –
Waziri wa Afya katika serikali ya kaunti ya Kilifi Charles Dadu amesema kaunti hiyo imewekeza kikamilifu katika miundo msingi ili kuboresha afya ya akina mama katika kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa halfa ya kupokea ufadhili wa vifaa mbalimbali vya kiafya kwa wadi ya akina mama ya kujifungua kutoka kwa wakfu wa Sportpesa katika hospitali ya Kilifi, Dadu amesema kaunti ya Kilifi imelipa kipau mbele swala la afya.
Waziri huyo amewataka wahudumu wa afya kudumisha uhusiano mwema kati yao na wagonjwa wanaofika hospitalini kutafuta huduma za matibabu.
Kwa upande wake msimamizi wa wadi ya akina mama ya kujifungua katika hospitali hiyo Janet Rotich amesema huduma za uzazi zitaboreshwa zaidi.