Story by Gabriel Mwaganjoni-
Huduma za utoaji chanjo dhidi ya virusi vya Corona katika hospitali kuu ya Hola kaunti ya Tanariver zimesitishwa kwa siku ya pili mtawalia baada ya chanjo elfu moja zilizokuwa katika hospitali hiyo kuisha.
Afisa mkuu wa kitengo cha chanjo hospitalini humo, Billsaid Mkamba amesema kufuatia amri ya Serikali kwamba wahudumu wa umma wapate chanjo kufikia tarehe 23 mwezi huu wa Agosti, chanjo hizo ziliisha kufikia siku ya Jumatatu juma hili.
Mkamba amesema hospitali hiyo ilipokea jumla ya chanjo elfu 1 siku la Alhamis juma lililopita japo ongezeko la watu waliohitaji kudungwa chanjo ndio iliyopelekea chanjo hizo kumalizika na hadi sasa hospitali hiyo ingali inakabiliwa na uhaba wa chanjo ya Corona.
Mkamba amesema kufikia sasa zaidi ya watu 3,000 wamedungwa chanjo hiyo akiongeza kwamba wanatarajia kupokea chanjo zaidi kutoka kwa Serikali ili zoezi hilo liendelee.