Tarehe 6 Oktoba 2018 kituo cha Radio Kaya kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la Plan International na Samba Sports Youth Agenda kilituza shule ya upili ya wasichana ya Kwale kwa kuibuka mabingwa wa ukanda wa Afrika Mashariki katika soka.
Kwale waliibuka mabingwa kwa kuilaza Kawempe kutoka Uganda kwa bao 1-0 kwenye fainali iliyochezwa tarehe 19 Agosti 2018 mjini Musanze, Rwanda.