Picha kwa Hisani –
Mwanamuziki nyota kutoka Pwani ya Kenya Ali Mohamed almaarufu Masauti amefunguka kuhusu sababu zilizomplekea kuacha shule kidato cha pili na kuingia katika sanaa ya muziki.
Masauti ameeleza kuwa aliguswa na jinsi mama yake alivyokuwa anateseka kuwatafutia mahitaji yao na akaamua kuwacha shule na kuwa msanii, jambo ambalo anadai halikumfurahisha mama yake.
“Nilikuwa kidato cha kwanza nikienda kidato cha pili, niliacha shule kwa maana niliona mama anateseka sana kututafutia lakini si kuacha kwa ubaya…
…Mama yangu ndiye alikuwa mama na baba wa nyumbani,baada ya kuacha shule niliamua kuingia katika muiki ambapo mama yangu hakufurahi sana.” – alieleza Masauti.
Mwanamuziki huyo pia ameeleza kulelewa na mzazi mmoja na kuwa baba yake hakuwahi kushughulikia matakwa yao kwa sababu alikuwa na mke mwingine. Hata hivyo, alisema kuwa hato mlaumu baba yake kwa lolote lile.
Baba hakuwa anatusaidia sana kwa maana alikuwa na bibi wengine, baba mwenyewe ndiye aijitia vitu vingi lakini kwa kweli siwezi mlaumu kwa lolote.” Alieleza Masauti.