Hisia mseto zimeibuka miongoni mwa wananchi kuhusiana na ongezeko la bei ya mafuta nchini.
Kulingana na mwanaharakati wa maswala ya kijamii katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa Moses Simiyu ongezeko hilo litawasababishia wakenya mzigo mkubwa kumudu gharama ya maisha.
Akizungumza mjini Mombasa Simiyu ameishinikiza serikali kuingilia kati na kupunguza bei hiyo kwa manufaa ya wananchi wake.
Kwa sasa lita moja ya mafuta ya petrol jijini Mombasa inauzwa kwa shilingi 124 kutoka bei ya awali ya shilingi 105 huku lita ya mafuta ya diseli ikiuzwa kwa shilingi 110 kutoka shilingi 95 nayo lita moja ya mafuta ya taa ikiuzwa shilingi 93 kutoka shilingi 70.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.