Jamii ya Warundi wanaoishi katika kaunti ya Kwale, wamesema hawatakata tamaa kwenye juhudi zao za kuishinikiza serikali kuwasajili kama raia wa Kenya.
Mwenyekiti wa jamii hiyo Shadrack Kiza Barnaba, amesema imekuwa vigumu kwao kupata huduma muhimu za serikali, bila kitambulisho cha kitaifa huku akielezea imani yake kwamba tatizo hilo litatatuliwa hivi karibuni.
Akiongea na mwanahabari wetu, Kiza amesema kwamba wanashirikiana na serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Kwale, ili kuona kwamba wanasajiliwa rasmi kama wakenya kabla ya uchaguzi mkuu ujao.
Mwenyekiti huyo aidha amedokeza kwamba watu wa jamii hiyo wamenza harakati za kujua idadi yao kamili , kwa kufanya mikutano inayowaleta pamoja warundi wanayoishi ukanda wa Pwani.
Taarifa na Michael Otieno.