Kadhi wa mahakama ya Kwale Salim Mwaito amesema hatua ya wanaume kutelekeza familia zao ni chanzo kikuu cha kuvunjika kwa ndoa nyingi.
Akizungumza na mwanahabari wetu afisini mwake,Mwaito amesema mwaka uliopita wa 2020 alipokea kesi 20 za wanandoa kutaka kutalakiana na kwamba tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi kufikia sasa amepokea jumla kesi 6.
Kadhi Mwaito aidha amewataka wanaume kuwajibikia majumu yao kama walivyokula kiapo wakati wa kufunga ndoa ili kuepuka ongezeko la talaka akiitaka jamii kutoa ushauri kwa wanandoa mara kwa mara.