Story by Our Correspondents-
Hatma ya Kinara wa Muungano wa Azimio la umoja One Kenya Raila Odinga ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa Agosti 9 iko chini ya Jopo la majaji 7 wa Mahakama ya upeo iwapo Muungano huo utawasilisha kesi Mahakamani kufikia siku ya Jumanne tarehe 23.
Ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kipindi cha kuwasilisha kesi ya kupinga matokeo ya urais kukamilika, Muungano huo umeshikilia kwamba unakamilisha kukusanya ushahidi.
Mawakili wa Muungano huo akiwemo Paul Otiende Amollo, wamedai kwamba wanautilia shaka ushindi wa Rais mteule Dkt William Ruto, na ukweli kuhusu ushindi huo utabainika wazi Mahakamani.
Hata hivyo Tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC imedai kwamba itawakilishwa Mahakamani na aliyekuwa mkuu wa sheria nchini Githu Muigai katika kesi hiyo huku ikishikilia kwamba uchaguzi huo ulikuwa huru na haki.
Kwa upande wake Muungano wa Kenya Kwanza huajaweka wazi majina ya mawakili watakaotetea ushindi wa Ruto katika Mahakama ya upeo huku japo viongozi wa Muungano huo wamesema wako tayari kujitetea Mahakamani.
Jopo hilo la majaji 7 linajumuisha Jaji mkuu nchini Martha Koome, Naibu wake Jaji Philomena Mwilu, Jaji Smokin Wanjala, Jaji Ibrahim Mohamed, Jaji Njoki Ndungu, Jaji William Ouko na Jaji Isaac Lenaola.