Wakaazi katika eneo bunge la Rabai kaunti ya Kilifi wamekabidhiwa zaidi ya hati miliki elfu tatu za mashamba yao kutoka kwa wizara ya ardhi nchini.
Akiongea wakati wa kukabidhi wakaazi vyeti hivyo Mbunge wa Rabai William Kamoti amezitaka familia zinazo miliki ardhi za pamoja kufanya mashauriano kabla ya kuuza ardhi hizo ili kuepuka mizozo.
Kwa upande wake Naibu kamishna kaunti ya Kilifi eneo la Rabai Jama Mahamud amesema ugavi wa hati miliki utapunguza visa vya mauji ya wazee akisema kuwa visa hivyo uchipuka kutokana na migogoro ya ardhi.
Wakaazi wa maeneo ya Mwawesa , Chang’ombe , Jimba, Maereni,na Pangani ni miongoni mwa walionufaika na hati miliki hizo.
Taarifa na Mercy Tumaini.