Picha kwa Hisani –
Seneta wa kakamega Cleophas malala ameachiliwa huru baada ya kuzuiliwa na maafisa wa polisi kwa zaidi ya masaa 36.
Malala hata hivyo hatowasilishwa mahakamani kama ilivyotarajiwa baada ya afisi ya mkurungezi wa mashtaka ya umma nchini ODPP kumuondolea mashataka yaliomkabili.
Akizungumza nje ya kituo cha polisi cha Mumias baada ya kuachiliwa Malala amelaumu maafisa wa polisi kwa kumuhangaisha akisema ataendelea kupinga mfumo mpya wa ugavi wa mapato kwa kaunti akiutaja kama kandamizi.
Kabla kuachiliwa huru wafuasi wa seneta Malala asubui ya leo wameandama na kuifunga barabara ya kakamega Kisumu wakishinikiza kuachiliwa huru kwa seneta huyo.
Wakili wa Malala, Nelson Havi ameshikilia kwamba ni lazima mkuu wa sheria nchini Paul Kihara,waziri wa usalama wa ndani Dkt fred Matiangi na inspekta Jenerali wa polisi nchini Hilary Mutyambai kufika mbele ya seneti hapo kesho kueleza kiini cha kuzuiliwa kwa maseneta wote watatu ambao kwa sasa wameachiliwa huru.