Story by Gabriel Mwaganjoni-
Hatimaye mwili wa marehemu Carol Wayua Mueni aliyekuwa akihudumu katika afisi ya Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir umezikwa.
Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Mbunge wa Mvita na Mwakilishi wa Wadi ya Shanzu Maimuna Salim, mwili wa Carol umefanyiwa ibada ya wafu katika ukumbi wa Ginnery Multi-Purpose mjini Kitui kabla ya kuzikwa katika maziara ya mji huo.
Nassir amemtaja Carol kama aliyekuwa muadilfu katika majukumu yake na kifo chake ni pigo kwake na familia yake hasa ikizingatiwa kwamba binti huyo alikuwa na umri wa miaka 24.
Carol alikuwa miongoni mwa wafanyakazi wengine Ali Naaman, Athman Mohammed na Ellison Musyoka waliyofariki tarehe 13 mwezi huu wa Novemba katika eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupasuka gurudumu na kugonga mlingoti wa stima kabla ya kubingiria mara kadhaa.
Tayari Naaman, Mohammed na Musyoka walizikwa siku iliyofuata ya Jumapili tarehe 14 ya mwezi huu wa Novemba katika desturi za dini ya Kiislamu, huku mwili wa Carol akihifadhiwa katika ya hospitali ya Pandya mjini Mombasa kabla ya kuzikwa huko Kitui.