Picha kwa hisani –
Mgomo wa madaktari umesitishwa hii leo alasiri baada ya mkutano kufanywa baina ya Wizara ya afya na viongozi wa chama cha madaktari nchini KMPDU.
Akizungumza na wanahabari Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe amesema baada ya mazungumzo yaliyohusisha viongozi wa chama cha madaktari nchini KMPDU na wizara hiyo madaktari walikubali kusitisha mgomo wao .
Waziri Kagwe ameeleza kuwa Wizara ya afya imekubali kutimiza matakwa ya madaktari ambayo ni kuwapa marupurupu ya kazi pamoja na vifaa vya kuzuia msambao wa Corona ikwemo bima ya matibabu.
Aidha mapema wiki hii madaktari waliungana na maafisa wa klinik pamoja na wauguzi kuendeleza mgomo ili kushinikiza kulipwa marupupu ya mshahara , kupewa vifaa vya kuzuia Corona pamoja na bima ya matibabu .