Shirikisho la soka nchini FKF limeingia katika mkataba na kampuni moja ya mchezo wa bahati nasibu humu nchini itakayokuwa mdhamni mkuu wa timu ya soka ya wanaume ya kitaifa, Harambee Stars.
Mkataba huo utaiona Harambee Stars ikipata ufadhili wa shillingi milioni 20 watakaposhiriki mechi za mchuano wa kuwania kombe la mataifa ya Afrika ( AFCON). Milioni 5 zimetengewa utengenezwaji wa jezi.
Harambee stars kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15 imefuzu kwa mchuano huo.
Tarehe 23 Machi inakabiliana na Ghana kwenye mechi ya mwisho ya kufuzu.
Taarifa na Dominick Mwambui.