Nahoda wa timu ya taifa Harambee Stars Victor Wanyama amewapatia matumaini wachezaji wenzake katika timu hiyo matumaini ya kufanya vyema kwenye mchuano wa AFCON mwaka 2019 kwa kufunga bao la ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Madagascar.
Harambee Stars waliandikisha ushindi wa 1-0 dhidi ya Madagascar kwenye mechi hiyo ya kirafiki iliyochezwa katika uwanja wa Robert Boban, nchini Ufaransa.
Harambee Stars ni miongoni mwa timu 24 zitakazoshiriki mchuano wa AFCON nchini Misri. Stars inarudi katika mashindano hayo baada ya miaka 14. Hii ni mara ya kwanza kwa Madagasar kushiriki mchuano huo.