Wanamuziki na hata ma-producer mbali mbali kutoka Pwani wameonyesha upendo wao kwa nahodha wa kipindi cha Kaya Flavaz Robert Matano maarufu kama Robby Dallaz, kwa kumtumia jumbe za heri njema hii leo katika siku yake ya kumbukumbu ya kuzaliwa kupitia mitandao ya kijamii.
Miongoni mwa wasanii hao ni pamoja na Ziky Mtanah, Bocar C, Fisherman, Fat-S, Adasa, C New, Mlole Classic, Mnyamwezi, Yuro Millionaire, Dogo Richie, Producer Emmy D,producer Shirko wa Shirko Media na wengine wengi.
Mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram na WhatsApp imepambwa na picha tofauti tofauti za Robby Dallaz ambae anajulikana hewani pia kwa majina ya ‘Mzee wa kitai’ au ‘Mzee wa tendere’ au ‘Mtoto wa pasta anaye pendaga madebe’. Hii ni kutokana na yeye kupostiwa na mashabiki wake wengi sana wakiwemo wasanii na hata producer.
Katika jumbe zao maridadi zilizojaa sifa kem kem za heri njema ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake, jambo moja lilijidhihirisha wazi, kwamba wanamuziki chipukizi na hata waliovuma zamani wanapenda kazi anayoifanya kwenye kiwanda cha muziki ya kukuza talanta mkoani bila ubaguzi wa aina yoyote.
Hata hivyo, mtangazaji huyo ambaye amefikisha umri wa miaka 28, ameeleza furaha yake na kuwashukuru wote waliomtakia siku ya kumbu kumbu njema ya kuzaliwa kwake hewani kupitia kipindi hicho na pia kupitia video ambayo ameichapisha kwenye mitandao yake ya kijamii.
Wasimamizi wa Radio Kaya pamoja na wafanyikazi wenzake, tunamtakia kumbukumbu njema ya kuzaliwa kwake na siku iliyojaa furaha na baraka tele za Mwenyezi Mungu.