Picha Kwa Hisani –
Wasanii wengi wamejitokeza mitandaoni na kumtakia heri njema ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtangazaji wa Radio Kaya Robert Matano maarufu Kama Robby Dallaz.
Mitandao ya kijamii imefurika na jumbe za sifa, shukrani na heri njema kwa mtangazaji huyo wa kipindi cha kaya Flavaz kila jumatatu Hadi Ijumaa kwanzia saa tatu hapa saa saba na Kali zetu kila jumamosi kwanzia saa nne asubuhi Hadi saa saba mchana.
Mtangazaji huyu ambaye ameshawai kuwa mwanamuziki akiwa na kundi la Durz na kuvuma kwa ngoma yao ya “Party kidogo” pia ameweka ujumbe maridadi kuhusiana na siku hii spesheli kwake na kutoka shukrani kwa mashabiki wake na wasanii hao waliompa shavu mitandaoni.
Kati ya wanamuziki waliompost ni pamoja na Mr Kilifi, Dully Melody, Lemmy K, Rama K Rapper, J Love, shepherd, prince Lucky, Producer Shirko, Dogo Richie, Yuro Millionaire, Happy C, Babsody na Nadi.
Sisi tunamtakia baraka za Mwenyezi Mungu anaposherehekea siku yake hiyo.