Taarifa na Charo Banda
Hali ya taaruki ingali imetanda katika eneo la Mnazini kule Tana Delta kaunti ya Tana River baada ya watu wanne kuuwawa na watu wasiojulikana na kisha miili yao kuteketezezwa.
Afisa Mkuu wa upelelezi wa jinai katika eneo hilo Charles Atei amesema kuwa maafisa wake tayari wameanzisha uchunguzi kufuatia mauaji hayo tata.
Afisa huyo aidha amewataka wananchi wajitokeze na habari muhimu ambazo zitasaidia upelelezi sambamba na uchunguzi ili waliotekeleza unyama huo wachukuliwe hatua kali za kisheria.
kwa upande wao wakazi wa eneo hilo walioshughudia tukio hilo wamezitaka asasi zote za kiusalama kufanya uchunguzi wa haraka ili kufichua kiini cha mauaji hayo.
Mapema jana baada ya tukio hilo kufanyika shughuli zan kawaida katika barabara kuu ya Garsen Hola zilisambaratika kwa takriban maasaa manane yali iliyopelekea polisi kufyatua risasi hewani sawia na vitoa machozi baada ya wakazi kufunga barabara hiyo.