Picha kwa hisani –
Halfa ya kuapishwa kwa Spika wa bunge la kaunti ya Nairobi Benson Mutura kuwa Kaimu Gavana wa kaunti hiyo kwa kipindi cha muda wa siku 60 kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mdogo ili kuchaguliwa Gavana mpya imeahirishwa.
Kuahirishwa kwa hafla hiyo kumetokana na hitalafu za mahali ambapo Mutura alifaa kuapishwa ili kushikilia nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Gavana wa Nairobi Mike Mbuvu Sonko kubanduliwa afisini kutoka na sakata mbalimbali ikiwemo kashfa za ufisadi.
Iwapo Spika Mutura atapishwa basi atashikilia nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba kutokana na kwamba kaunti ya Nairobi imesalia kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili bali ya Naibu Gavana.
Gavana Sonko ni gavana wa pili nchini kutimuliwa madarakani baada ya aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu kubanduliwa uongozi.