Picha kwa Hisani –
Idara ya usalama katika Kaunti ya Mombasa imesema kuwa haitamsaza yeyote atakayekiuka amri iliowekwa na serikali ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku.
Mshirikishi mkuu wa Utawala Kanda ya Pwani John Elungata amesema Maafisa wa usalama watamkabili yeyote atakayekiuka amri hiyo akisema baadhi ya wakaazi na viongozi hasa katika Kaunti ya Mombasa wanakiuka sheria hiyo.
Elungata amesisitiza kwamba masharti yote yaliyotolewa na Rais Uhuru Kenyatta ikiwemo kusitishwa kwa uuzaji pombe katika mikahawa yanapaswa kuzingatiwa kikamilifu.