Picha kwa hisani –
Shirika la huduma za feri limeweka wazi kwamba halijamlazimisha mkaazi yeyote kutumia daraja la Liwatoni,japo hali hiyo hutokea wakati kivuko cha feri cha Likoni kinapokumbwa na hali tata.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Khamis Bakari Gowa amesema wakaazi wengi kwa sasa wanatumia kivuko hicho sawa na daraja hilo la Liwatoni ili kuvuka upande wa pili.
Hata hivyo, Gowa amelitaja daraja la Liwatoni kama afueni ,kwani wakaazi wameondolewa dhiki za kusubiri feri sawa na kuepuka msongamano.