Story by Taalia Kwekwe-
Huku maadhimisho ya siku 16 za uanaharakati yakiendele kote ulimwenguni, Hakimu mkuu wa Mahakama ya Kwale Lilian Lewa amesema ongezeko la kesi za dhulma za kijinsia Mahakamani zimechangiwa na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumza na Wanahabari Lilian amesema kuendelea kushuhudiwa kwa kiangazi kikali katika jamii kumepelekea familia nyingi kusambaratika na kusababisha watoto kuathiriki kimasomo.
Hakimu Lilian ameishinikiza serikali ya kaunti kuzisaidia familia zilioathirika na baa la njaa hasa kwa kuwajengea mabwawa ya maji sawa na kuwapa mafunzo kuhusu mimea inayostahimili kiangazi ili kuzalisha chakula.
Vile vile amewahimiza wazazi kuwaelimisha watoto wao kuhusu jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo katika jamii.