Shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika limeitaka serikali kuanzisha ubomozi wa nyumba zilizojengwa kwenye ardhi za umma katika kaunti ya Mombasa.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Hussein Khalid, amesema kuwa nyumba zilizojengwa kwenye ardhi za umma ndani ya kaunti hiyo zimetatiza utekelezwaji wa maendeleo kwa wakaazi.
Shirika hilo aidha limetishia kuwasilisha kesi mahakamani endapo serikali ya kitaifa na ile ya kaunti ya Mombasa haitatekeleza ubomozi huo.
Taarifa na Cyrus Ngonyo.