Shirika utetezi wa haki za kibinadamu la Haki Afrika limeitaka idara ya usalama kaunti ya Mombasa kuyakabili kikamilifu makundi ya vijana wadogo yanayoendeleza uhalifu kwa kutumia silaha butu na kuwapora wananchi mali zao.
Akizungumza na Wanahabari mjini Mombasa, Afisa wa kitengo cha dharura katika Shirika hilo Mathias Shipeta amesema makundi mengi ya vijana wahalifu katika kaunti hiyo yanajificha mashinani na kuna haja ya idara hiyo kuyakabili.
Shipeta amewataka maafisa wa polisi kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria kwa kuhakikisha wanawatia nguvuni wahalifu ili kuzuia ukiukaji wa haki za kibinadamu.
Hata hivyo amewataka vijana kudumisha amani na kujitenga na uhalifu, akisema Shirika hilo tayari limeanzisha zoezi la kuwahamasisha vijana wa mashinani kuhusu kudumisha amani.
Taarifa na Hussein Mdune.