Shirika la kutetea haki za kibinadamu la Haki Afrika limesema limeghadhabishwa na kitendo cha wizara ya elimu kwamba huenda takribani ya watahiniwa 400,000 wa darasa la nane kutosajiliwa na baraza la mitihani nchini KNEC kwa kukosa vyeti vya kuzaliwa.
Kulingana na Afisa wa kitengo cha dharura katika shirika hilo Mathius Shipeta ameitaja hatua hiyo kama ukiukaji wa Haki za elimu kwa watoto.
Hata hivyo Amesema kuwa nijukumu la serikali kubuni mbinu mbadala ya kutatua tatitizo hilo kwani amesema idadi kubwa ya wanafunzi hususani mashinani wanapitia changamoto nyingi kupata cheti cha kuzaliwa.
Haya yanajiri baada ya wizara ya elimu nchini kutoa orodha ya watahiniwa 370 ,000 ambao maomba yao kusajiliwa na baraza la KNEC yalikataliwa huku tatehe ya usalili itarajiwa kumalizika kesho.
Taarifa na Hussein Mdune.