Shirika la utetezi wa haki za kibinadamu la Haki Afrika limeapa kuwachukulia hatua za kisheria maafisa wa usalama wanaowahangaisha wakaazi wa vijiji vya Chira na Bilisa katika kaunti ya Tana river kufuatia oparesheni ya kiusalama inayoendelezwa na maafisa hao.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid amesema baadhi ya wakaazi wa vijiji hivyo wamedhulumiwa haki zao na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Minjilla licha ya baadhi yao kuwa akina mama walio na watoto wachanga na wengine wakongwe.
Khalid amesema tayari shirika hilo limetuma maafisa wake nyanjani ili kuidhinisha uchunguzi kuhusiana na dhulma hizo kabla ya kuwasilisha kesi rasmi mahakamani.
Oparesheni hiyo inatekelezwa baada ya raia wa Kitaliano Sylvia Romano kutekwa nyara takriban mwezi mmoja uliyopita katika kijiji cha Chakama eneo la Malindi kaunti ya Kilifi.
Tarifa Gabriel Mwaganjoni.