Shirika la kutetea wa haki za binadamu nchini la Haki Africa, limeishtumu vikali Wizara ya fedha kwa kuongeza asilimia 16 kwa bidhaa za mafuta humu nchini.
Kulingana na Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo Hussein Khalid, kuna haja ya hatua hiyo kusitisha kwani itamukandamiza mlipa ushuru na kuongeza gharama ya maisha kwa mwananchi wa kawaida.
Akizungumza mjini Mombasa, Khalid amesema tayari wakenya wanahangaika na kupanda kwa gharama ya maisha hivyo basi akaitaka serikali kuidhinisha njia mbadala ya kupata fedha za kufadhili miradi na wala sio kuwanyanysa wakenya.
Wakati huo uo amedai kuwa serikali inafaa kufanya mazungumza na wale waliopeana madeni humu nchini ili kuzikabili changamoto hizi badala ya kuwakandamiza wakenya kupitia njia ya kuwatoza ushuru wa juu.
Taarifa na Hussein Mdune.