Aliyekuwa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga, ameagiza kuanzishwa kwa uchunguzi wa haraka wa mauaji wa kijana mmoja katika eneo la Kajado, Kaloleni kaunti ya Kilifi.
Gunga amesema visa vya mauaji ya kiholela ambayo yanadaiwa kutekelezwa na watu wasiojulikana vinafaa kusitishwa mara moja.
Akizungumza na Mwanahabari wetu kwa njia ya simu, Gunga amewataka wakaazi kushirikiana vyema na maafisa wa polisi na kutoa habari zitakazopelekea kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.
Kwa upande wake Naibu Chifu wa eneo la Mrimani huko Kaloleni, Samuel Jali Karisa ameshtumu mauaji hayo, akisema iwapo kuna maswala tata ambayo huchangia visa vya mauaji basi yanafaa kujadiliwa kupitia mazungumzo.
Taarifa na Mercy Tumaini.