Wakili Gunga Mwinga amezitaka idara za Mahakama nchini kuajiri wafanyikazi maalum watakao tumika kutafsri lugha za watu wanaoishi na ulemavu kwenye mahakama za humu nchini.
Akiongea mjini Mombasa Gunga amesema kuwa hatua hiyo itasaidia pakubwa kurahisisha walemavu wengi kutambua kwa urahisi kesi zinapoendelea sawia na kuzifuatia kwa urahisi .
Aidha Amesema kuwa idadi kubwa ya kesi za walemavu zinacheleweshwa mahakamani kutokana na changamoto hiyo.
Taarifa na Hussein Mdune.