Aliyekuwa Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga amewataka wanaogawa chakula cha msaada kuhakikisha kuwa kinawafikia waathiriwa wa baa la njaa.
Kulingana na Mwinga mara nyingi chakula hicho hakifikii familia ambazo zimeathirika hatua anayoitaja kuongeza gharama ya maisha.
Gunga hata hivyo amewataka viongozi kukoma kutumia swala la ugavi wa chakula cha msaada kujipigia debe kisiasa na badala yake kuhakikisha chakula hicho kinawafaidi wakaazi walioathirika.
Wakati uo huo ameitaka serikali ya Kilifi na wawekezaji kujizatiti kuhakikisha chakula kinasambazwa kwa maeneo ya mashinani ambayo yameathirika zaidi ndani ya kaunti hiyo.
Taarifa na Hussein Mdune.