Story by Our Correspondents-
Seneta wa kaunti ya Lamu Joseph Githuku amesema iwapo viongozi wa kaunti ya Lamu watashirikiana vyema basi tatizo la mzozo wa ardhi katika kaunti hiyo litapata suluhu.
Akizungumza mjini Hindi katika kaunti hiyo, Githuku amewahakikishia wakaazi wa kaunti hiyo kwamba swala hilo tata litapata suluhu la kudumu.
Githuku amesema mikakati hiyo tayari inaendelea ili kuhakikisha wakaazi wa kaunti hiyo hawasumbuliwi tena na mabwenyenye na badala yake waishi katika ardhi zao bila ya usumbufu.
Wakati uo huo ametoa wito kwa serikali ya kaunti ya Lamu kulipa kipaumbele swala la ugavi wa ardhi kwa wenyeji ili kukomesha matumizi mabaya ya swala la ardhi na wanasiasa.