Story by Gabriel Mwaganjoni-
Mgombea huru wa ubunge wa Nyali Eric Gitonga amehoji kwamba atabadilisha mtindo wa kufanya kazi na vijana katika eneo hilo ili vijana wa Nyali wanufaike kimapato na miradi mbalimbali itakayotekelezwa katika eneo hilo.
Gitonga amesema sio vigumu kuwashirikisha vijana katika mchakato wa kimaendeleo na kuhakikisha wananufaika kimapato, japo ni sharti vijana hao watambuliwe na kuhusishwa kikamilifu.
Akizungumza katika eneo la Kongowea alipokuwa akiendeleza kampeni zake za kisiasa, Gitonga amesema bila ya kumhusisha kijana katika mchakato wa maendeleo basi unamsukuma kijana huyo katika kutumiwa na wanasiasa ili azue vurugu au kujihusisha na uraibu wa dawa za kulevya.
Hata hivyo, amewataka vijana kujitenga na wanasiasa wachochezi na badala yake kukumbatia kampeni za amani.