Mwanamuziki wa Bongo Flava na video vixen Gift Stanford maarufu kama Gigy Money ameelezea kuudhika na hatua ya muigizaji maarufu kutoka Tanzania Wema Sepetu kutoudhuria shuguli yake aliyoiandaa ya kusherekea siku yake ya kuzaliwa. Gigy alitoa mwaliko kwa baadhi ya watu wake wa karibu akiwemo Wema Sepetu kwa sherehe hiyo iliyofanyika tarehe 16 mwezi huu.
Kupitia mahojiano ya moja kwa moja na kituo kimoja cha habari mjini Dar Es Salaam, nchini Tanzania, msanii huyo alilalamikia mastaa anaowapenda akiwemo Wema kutofika kwenye sherehe yake hata baada ya kumnunulia pombe yenye bei ghali na kusema kwamba wanamuona kutokuwa hadhi kama yao.
“About Wema umenikumbusha, hivi dada Wema kuna tatizo? Wajua mimi ni mtu ambaye sijui labda… and by the way, you know what, that’s why I love to live on my line. You know what bro? I love these people, I love them and I cannot change that but may be they see me I’m not their standard. Wameanza muda and you know, everyone has their reasons…” – Gigy Money
Gigy pia alieleza jinsi alivyokuwa mtu wa kwanza kufika katika sherehe ya siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Wema Sepetu ambayo ilifanyika mwezi septemba mwaka jana na kumlipia meza aliyokaa Wema siku hiyo.
“Nimewaalika kwa sababu last birthday ya Wema I was there and nakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kufika location. I was the one that nili reserve table for her even if it was her birthday to make things right, so I feel very disappointed…” – Gigy Money
Hata hivyo, Gigy aligeuka kuwa mwenye furaha baada ya kuonyeshwa ujumbe ulioandikwa na Wema Sepetu kupitia ukurasa wake wa Instagram, alipokuwa anaendelea na mahojiano hayo, wa kumtakia heri njema kwa sherehe yake na kumuomba radhi ya kutofika kwani wangezungumza zaidi baadae.
“Happy Birthday to my Babysis Gift… Babygirl you are a superstar… You were born to shine in all directions… You are a Unique Gem and I want you to let your light overcome all shadows… Cause you got it sugar…!!! I love you so much… But set life has been getting the best of me… I will make it up to you I promise… Alafu nakudai… Naomba tukutane inbox basi… Nakupenda sana…” – Wema Sepetu