Story by Salim Mwakazi –
Kinara wa chama cha KANU Gideon Moi ameanza ziara yake ya kisiasa katika ukanda wa Pwani ili kujipigia debe katika kinyang’anyiro cha urais wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.
Akizungumza katika eneo la Diani kaunti ya Kwale, Gideon amesema siasa za mwaka wa 2022 zitakuwa za kuwaunganisha wakenya wote huku akiwataka wanachama wa chama hicho kujitokeza na kuwania nyadhfa mbalimbali za uongozi.
Gideon amesema mikakati ya chama hicho itaendelezwa kote nchini ili kuhakikisha chama hicho kiko imara huku akidai kwamba viongozi wote wa Muungano wa One Kenya Alliance wanalenga kumjumuisha Odinga.
Hata hivyo wandani wa Gideon Moi akiwemo Mwakilishi wa Kike kaunti ya Lamu Captain Ruweida Obo, Mbunge wa Fafi Garissa Abdikarim Osman, Mwanasiasa Gereza Dena, na Mwakilishi wa wadi ya Mwereni Manza Beja wamewataka wananchi kumuunga mkono Gideon katika kinyang’anyiro cha urais.
Siku ya Alhamis Gideon anatarajiwa kukutana na viongozi wa chama cha KANU katika kaunti ya Mombasa kabla ya mkutano mkuu unatarajiwa kufanyika jijini Nairobi katika ukumbi wa Bomas.