Ally B, msanii aliyevuma kwa vibao motomoto hapo awali kama vile; Mariah, Bembea,Kadzo miongoni mwa vibao vingi tu, kisha ghafla akapotea kwenye ‘game’ …Mashabiki na washika dau wa muziki wa kizazi kipya kanda ya Pwani walimiss sana Flavour ya muziki wake lakini hakuna aliyefahamu siri ya msanii huyu ilikuwa ni nini.
Baada ya hayo yote,Ally B aliamua kuvunja ukimwa na kurudi studioni lakini safari hii akiwa na rafiki yake wa jadi aliyekuwa kijana wake wa mkono wakati huo katika shughuli za uimbaji,walikaa chini katika Recording studio ya Kay-G Records & Kay-G Films chini ya uongozi wa Prodiuza Totti,na kuamua kufanya bonge la track iliyokwenda kwa jina la GENYE GENYE – Aliomshirikisha kijana wake wa jadi almaarufu, Masauti a.k.a Kenyan Boy.
Baada ya audio kutrend midomoni mwa washika dau wa muziki wa Pwani,pamoja na mashabiki, Ally B na Masauti waliamua kufanya bonge la video chini ya ufadhili wa Radio tajika/na maarufu zaidi katika mkoa wa Pwani RADIO KAYA. Baada ya video kukamilika chini ya ufadhili wa RADIO KAYA,Mkurugenzi wa kituo hiki aliamua kufanya tamasha kubwa la ku launch video hii katika Club Lambada – Mtwapa.
Baada ya tamasha la uzinduzi wa video hii kukamilika,Ally B alipata umaarufu zaidi nchini kwa kupata mialiko katika vituo vya redio na vituo vya runinga kote nchini na hata nchi jirani. Kulingana na Ally B – Genye Genye ndio wimbo pekee uliomtambulisha zaidi Afrika. “Hakika Genye Genye ilikill” Ally B akifunguka.