Picha kwa hisani –
Gavana wa Nyamira marehemu John Nyagarama anatarajiwa kuzikwa hii leo na tayari ibada ya mazishi inaendelea katika shule ya msingi ya Nyamira.
Viongozi mbali mbali akiwemo aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga,jaji mkuu David Maraga, mawaziri,magavan,wabunge ,wawakilishi wadi na viongozi wengine tayari wamewasili katika hafla hio ya mazishi inayoendelea kwa sasa katika kaunti ya Nyamira.
Viongozi waliohudhuria hafla hio kwa sasa wanaendelea kutoa hotuba zao
Mwendazake Nyagarama aliaga dunia wiki moja iliyopita akiwa na umri wa miaka 74 ,akiwa katika hospitali ya Nairobi ,baada ya kupata maambukizi ya virusi vya corona.
Nyagarama ni gavana wa kwanza nchini kuaga dunia kutokana na maambukizi ya virusi vya corona.