Picha kwa hisani –
Viongozi mbali mbali nchini wametuma rambi rambi zao kwa jamaa wa mwendazake gavana wa Nyamira John Nyagarama aliyeaga dunia asubui ya leo akiwa na umri wa miaka 74.
Kiongozi wa hivi punde kutuma rambi rambi zake ni rais Uhuru Kenyatta ambae amemtaja mwendazake kama kiongozi aliyechangia maendeleo ya taifa hasa kupitia sekta ya majani chai.
Kwa upande wake Naibu wa rais William Ruto na mwenzake kinara wa ODM Raila Odinga wamemtaja mwendazake Nyagarama kama kiongozi aliyejizatiti kuuimarisha ugatuzi.
Familia ya marehemu imebainisha kwamba kiongozi huyo ameaga dunia katika hospitali ya Nairobi,na alikua amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi kwa wiki kadhaa,na tayari mwili wake umepelekewa katika hifadhi ya maiti ya Lee jijini Nairobi.