Picha kwa hizsani –
Gavana wa kaunti ya Machakos Daktari Alfred Mutua ametangaza rasmi kuwa atawania urais mwaka 2022 kupitia chama chake cha Maendeleo Chapu Chapu.
Akizungumza na wanahabari katika Kaunti hiyo gavana Mutua amesema wakenya wamechoka na tamaa ukabila na ufisadi unaotekelezwa nchini na baadhi ya viongozi walio mamlakani.
Gavana huyo wa Machakos amewahakikishia wakenya mwamko mpya kupitia kubuni fursa za ajira.
Mutua amesema taifa la kenya kwa wakati mmoja lilikuwa sawa kiuchumi na mataifa kama vile Korea Kusini na Malaysia ambayo kwa sasa yemepiga hatua kubwa kimaendeleo .
Kiongozi huyo wa chama cha maendeleo chapa chapa amesema iwapo wakenya hawatabadili jinsi wanavyochagua viongozi basi taifa hili litaendelea kusalia nyuma kiuchumi.