Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amepinga vikali mfumo mpya wa ugavi wa mapato unaolengwa kutekelezwa kwa serikali za kaunti, akisema huenda ukaathiri pakubwa maendelea ya kaunti.
Gavana Mvurya amesema iwapo mfumo huo utaidhinishwa na bunge la seneti jinsi Tume ya ugavi wa mapato nchini inavyopendekeza basi kaunti ya Kwale itapoteza takribani shilingi bilioni 1.2.
Akizungumza na Wanahabari, Gavana Mvurya amedai kuwa hatua hiyo itaathiri pakubwa shughuli za maendeleo katika serikali za kaunti nchini.
Wakati huo uo Gavana Mvurya amewataka maseneta kuupanga mfumo huo bungeni kwani utahujumu shughuli nyingi za maendeleo mashanani na malengo ya Katiba ya nchi.
Mfumo huo mpya wa ugavi wa mapato kwa serikali za kaunti nchini umezua mdahalo huku Maseneti kutoka kanda ya Pwani wakishikilia kutounga mkono mfumo huo mpya kwani utalemeza juhudi za maendeleo mashinani.