Huenda wakazi wa kaunti ya Kilifi walijipata matatani baada ya Serikali ya kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na ile ya Kitaifa kutoa masharti mapya dhidi ya janga la Corona katika kaunti hiyo.
Gavana wa Kilifi Amason Jefa Kingi amesema hakuna maiti itakayotolewa wala kuzikwa katika kaunti hiyo bila ya maafisa wa polisi kufahamu la sivyo familia iliondokewa na mpendwa wao italazimika kuwekwa karatini kwa siku 14 chini ya gharama zao.
Kingi ameteta vikali kutokana na tabia ya wakaazi kupenda kubugia pombe ya Mnazi kwa kukongamana mahali pamoja kutokana na tabia ya kupuuza kuwepo kwa janga la Corona nchini.
Hii ni baada ya kubainika kuwa kumekuwa na ukiukaji mkubwa wa maagizo ya serikali kuhusu mazishi wakati huu wa vita dhidi ya Corona.