Picha kwa Hisani –
Mahakama ya milimani imemuachilia gavana wa Garissa Ali Korane kwa pesa taslimu shilingi milioni 3.25 ama dhamana ya shilingi milioni tano baada ya kukanusha shutuma za ufisadi zinazomkabili.
Akitoa uamuzi huo hakimu mkuu wa mahakama hio Douglas Ogoti pia amemtaka Korane kutofika afisini mwake hadi pale kesi hio itakapoamuliwa sawa na kuwasilisha cheti chake cha usafiriki katika mahakama hio.
Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hio naibu mkurugenzi wa mashataka ya umma nchini Alexander Muteti ameitaka mahakama hio kumuwekea vikwazo gavana huyo iwapo ataachiliwa kwa dhamana.
Mawakili wa Korane akiwemo Ahmednassir Abdhulah na Paul Nyamodi hata hivyo wameshikilia kwamba hakuna ushahidi unaonyesha kwamba Korane na familia yake walinufaika na fedha hizo za maendeleo zinazodaiwa kufunjwa.
Korane na maafisa wengine wanne wa kaunti ya Garissa wanatuhumiwa kwa kufuja shilingi milioni 233.6 fedha zilizotolewa na benki ya dunia kuidhinisha miradi maendeleo katika kaunti hio.