Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Taita taveta Granton Samboja, amechaguliwa rasmi kuwa Mwenyekiti mpya wa jumuiya ya kaunti za Pwani.
Akizungumza baada ya kikao cha pamoja cha magavana wa kaunti za Pwani kilichoandaliwa katika kaunti ya Taita taveta, Gavana Samboja amesema lengo kuu la jumuiya ya kaunti za Pwani ni kuziunganisha kaunti zote za pwani pamoja kimaendeleo.
Gavana Samboja amesema Magavana wote wa eneo la Pwani wamekubaliana kuungana na kupigania maslahi ya wakaazi wa Pwani kwa kuhakikisha wanajumuishwa katika meza ya mazungumzo na serikali.
Wakati uo huo, amedai kuwa kama magavana wa kaunti za Pwani wameungana kuhakikisha eneo la Pwani linatambulika kikamilifu katika ngazi ya kitaifa huku akidai kuwa ni wakati wa viongozi kutoka maeneo mengine ya nchi kuunga mkono ajenda yao.
Hata hivyo Magavana wa kaunti za Pwani waliohudhuria kikao hicho ni Pamoja na Gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, Gavana wa Tana river Ghadho Godhana, Gavana wa Lamu Fahim Twaha, pamoja na Gavana wa Kilifi Amason Kingi.