Picha Kwa Hisani
Gavana wa Migori Okoth Obado pamoja na wenzake 9 wakiwemo watoto wake watatu wamejisalimisha mbele ya maafisa wa tume ya EACC huko Kisii kuandikisha taarifa kuhusu madai ya wizi wa shilingi milioni 73.4 fedha za kaunti.
Obado na washukiwa wenzake wakiwemo maafisa wa kaunti ya Migori na wafanyibiashara wanaohusika katika sakata hio watawasilishwa mahakamani jijini Nairobi kujibu mashtaka yanayowakabili.
Siku ya jumanne juma hili mkurugenzi mkuu wa mashataka ya umma nchini Noordin Hajj aliweka wazi kwamba ameridhishwa na uchunguzi uliofanywa na Tume ya EACC na yuko tayari kufungua mashtaka dhidi ya Obadona wenzake.
Uchunguzi wa maafisa wa EACC umebainisha kwamba Obado alipokea shilingi milioni 73.4 kupitia kampuni za wandani wake kati ya mwaka wa kifedha wa 2013/14 na mwaka wa kifedha wa 2016/2017.