Story by Bakari Ali-
Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir ametuea kuteua rasmi baraza lake la mawaziri.
Katika barua rasmi iliyotumwa kwa vyombo vya habari na kuwasilishwa mbele ya bunge la kaunti ya Mombasa, Nassir ameteuwa baraza lake la mawaziri la watu 10 huku akimteuwa Naibu Gavana wa kaunti hiyo Francis Thoya kama Waziri wa Mazingira.
Dkt Mbwarali Kame ameteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na masuala ya kidijitali, Evans Oanda kama Waziri wa fedha na masuala ya kiuchumi, Swabah Ahmed akiteuliwa kuwa Waziri wa Afya naye Daniel Otieno akipewa Wizira ya uchukuzi na miundo msingi.
Wengine ni pamoja na Emily Achieng aliteuliwa kuwa Waziri wa Maji, madini na mabadiliko ya tabia nchi, Kenneth Muigai kama Waziri wa masuala ya vijana na michezo, Kibibi Abdallah akiteuliwa kama Waziri wa Kilimo, mifugo na masuala ya uchumi samawati, Mohammed Osman kama Waziri wa Utalii, biashara na utamaduni huku aliyekuwa msaidizi wake wa kibinafsi Mohammed Hussein Mohammed akiteuliwa kama Waziri wa ardhi, nyumba na ustawishaji wa kaunti hiyo.
Nassir vilevile amemteuwa Dkt Noah Akala kama mkuu wa wafanyakazi katika serikali ya kaunti hiyo naye Mahmoud Noor akiteuliwa kama mshauri wake mkuu sawia na mshauri katika masuala ya teknolojia na uvumbuzi.