Serikali ya kaunti ya Kwale imeahidi kuboresha mikakati yake ya kulinda mipaka hasa katika eneo la Lungalunga kwenye mpaka wa Kenya-Tanzania ili kuzuia maambukizi ya Corona.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema juhudi hizo pia itawekwa katika mpaka wa kaunti hiyo na Mombasa huku akiwataka wakaazi wa Kwale kukumbatia juhudi za kuzuia maambukizi hayo.
Wakati uo huo amedokeza kuwa serikali ya kaunti hiyo kwa ushirikiano na wadau wa kiafya inalenga kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi huku akiahidi kuwa wahudumu wa afya pia watapata vifaa vya kujikinga na virusi hivyo.