Picha kwa hisani –
Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amewakosoa baadhi ya viongozi ambao wanapiga vita mradi wa elimu ni sasa unaotekelezwa na Serikali ya kaunti hiyo.
Gavana Mvurya amesema lengo la kufadhili mpango wa masomo kwa wanafunzi kupitia basari ni kuhakikisha wanafunzi wanaotoka familia maskini wanapata fursa ya kujiendeleza kimasomo.
Akizungumza na wanahabari mjini Kwale, Mvurya amesema mpango huo wa masomo utaboresha maisha ya Kwale na kupambana na umaskini.
Wakati uo huo amemkashifu vikali Seneta wa kaunti ya Kwale Issa Boi kwa madai ya kuendeleza siasa za kuupiga vita mpango huo wa elimu.