Picha kwa hisani –
Serikali ya kaunti ya Kwale imewaagiza wahudumu wote wa afya wanaoshiriki mgomo katika kaunti ya Kwale kurudi kazini mara moja na kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji huduma za matibabu.
Gavana wa Kwale Salim Mvurya amesema sio vyema kwa serikali ya kaunti hiyo kuendelea kuwalipa mshahara wahudumu wa afya na maafisa wa kliniki huku wakishiriki mgomo kutokana na mshukumo kutoka kwa viongozi wao wa vyama.
Akizungumza na Wanahabari, Gavana Mvurya amesema matakwa ya wahudumu hao alitekelezwa baada ya mazungumzo ya kina, ni itakuwa makosa wakiendelea kushiriki mgomo ilhali serikali ya kaunti ya Kwale imetambua matakwa yao.
Mvurya ameeleza kwamba tayari serikali ya kitaifa kupitia wizara ya afya inatafuta mwafaka dhidi ya changamoto zinazowakumba wahudumu hao zilizopo katika ngazi hio ya kitaifa.
Hata hivyo mgomo wa wahudumu wa afya nchini umeingia juma la sita sasa huku serikali ikikosa kuwaewana na viongozi wa vyama vya wahudumu wa afya nchini kusuluhisha matakwa yao.