Story by Janet Shume –
Gavana wa kaunti ya Kwale Salim Mvurya amesema hakuna miradi yoyote itakayozinduliwa katika kaunti ya Kwale hadi wakaazi walioathirika na miradi mbalimbali watakapopata fidia zao.
Akizungumza katika kikao na wadau mbalimbali wanaohusika na mradi wa ujenzi wa bwawa la Mwache ikiwemo maafisa kutoka benki kuu ya dunia pamoja na Wizara ya maji nchini, Mvurya amesema ni lazima suala la fidia litekelezwe.
Mvurya amesema maafisa kutoka benki kuu ya dunia pamoja na wizara ya maji nchini wanatarajiwa kutembelea eneo hilo la mradi ili kutathmini changamoto pamoja na mafanikio ya mradi huo unaotarajiwa kuwanufaisha wengi.
Kwa upande wake afisa kutoka Wizara ya maji anayesimamia mradi huo Simon Mwangi amesema wataendelea kushirikiana na serikali ya kaunti ya Kwale ili kuhakikisha changamoto zinazoukabili mradi huo zinatatuliwa.