Story by Mercy Tumaini-
Huenda wakaazi wa eneo bunge la Kaloleni katika kaunti ya Kilifi wakazikabili changamoto za kiafya baada ya serikali ya kaunti hiyo kufungua rasmi wadi mbili za akina mama wanaojifungua katika hospitali ya Mariakani.
Akizungumza baada ya ufunguzi huo, Afisa mkuu wa matibabu katika hospitali hiyo Daktari Matano Kibwana amesema hatua hiyo imepandisha hadhi ya hospitali hiyo.
Kibwani amesema wadi hiyo ina vitanda 45 vya kuwalaza akina mama waliyojifungua na vitanda vingine 64 vya kuwalaza akina mama na watoto walio na matatizo tofauti.
Kwa upande wake Gavana wa kaunti hiyo Amason Jefwa Kingi ameahidi kuendeleza juhudi za kuboresha huduma za matibabu katika kaunti ya Kilifi huku akidokeza kuwa serikali yake inalenga kutengeneza chumba cha kufanyia upasuaji.