Story by Mwahoka Mtsumi –
Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Jefwa Kingi amevuliwa wadhfa wa Mwenyekiti wa chama cha ODM katika kaunti ya Kilifi na wadhfa huo ukakabidhiniwa Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire.
Kingi amevuliwa wadhfa huo na Baraza la kitaifa la chama cha ODM kutokana na madai ya kuandaa mikakati ya kubuni chama chake cha kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu ujao sawia na kuenda kinyume na sheria za chama.
Akizungumza na Wanahabari, Gavana Kingi ameshukuru uamuzi huo huku akikitia mema chama hicho wakati wa uchaguzi mkuu , akisema mipango ya kubuni chama cha Pwani cha kitaifa ni kuwaunganisha wapwani wote.
Kwa upande wake Mwenyekiki mpya wa Chama hicho katika kaunti ya Kilifi ambaye pia ni Mbunge wa Ganze Teddy Mwambire ameahidi kuendeleza mikakati ya chama hicho katika kaunti ya Kilifi huku akisema bado Gavana Kingi ni mwanachama wa ODM.